ULEGA AWASILI TABORA KUKAGUA MIRADI YA MIUNDOMBINU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 26, 2026

ULEGA AWASILI TABORA KUKAGUA MIRADI YA MIUNDOMBINU


Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, amewasili mkoani Tabora leo, Septemba 26, 2026, kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu inayotekelezwa na Sekta ya Ujenzi mkoani humo.

Akiwa mkoani Tabora, Waziri Ulega atakagua miradi mbalimbali ya barabara na miundombinu mingine inayotekelezwa katika mkoa huo, ili kujionea maendeleo ya miradi hiyo, pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wake.

Waziri Ulega ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde; Mkurugenzi wa Matengenezo kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Lazaro Loshirai, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na TANROADS.






No comments:

Post a Comment