Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Yusuf Masauni, amelitambua na kulipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa nafasi yake muhimu kama Mlezi na mdau wa kitaasisi wa Tanzania Green Summit.
Akizungumza Septemba 15, 2026 wakati wa ufunguzi wa Tanzania Green Summit 2026, Waziri Masauni amesema nafasi hiyo inaakisi dhamana ya NEMC katika usimamizi bora wa mazingira kupitia utekelezaji wa Sheria za Mazingira, Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ukaguzi, tafiti, uhamasishaji wa umma na uratibu wa masuala ya mazingira.
Waziri Masauni amesema Tanzania ina fursa kubwa katika nishati jadidifu, kilimo endelevu, nishati safi ya kupikia, uchumi wa mzunguko, uhifadhi wa mazingira, usimamizi wa taka na uchumi wa buluu, ambazo zinapaswa kugeuzwa kuwa thamani ya kiuchumi, ajira na maendeleo kwa wananchi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa vijana katika agenda ya mazingira na tabianchi, akiwataka kutambuliwa kama wabunifu, wajasiriamali, watafiti na viongozi wa baadaye wa uchumi wa kijani. Amehimiza kuwaunganisha vijana na ujuzi, teknolojia, mitaji, ushauri wa kitaalamu na masoko ili kuwawezesha kupata ajira na kukuza biashara.












No comments:
Post a Comment