KAMATI YA BUNGE YALIPONGEZA SUMAJKT KWA UBUNIFU WA UZALISHAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 24, 2026

KAMATI YA BUNGE YALIPONGEZA SUMAJKT KWA UBUNIFU WA UZALISHAJI


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Najma Murtaza Giga (Mb), imetembelea Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Mgulani, jijini Dar es Salaam, na kupongeza ubunifu wake katika uzalishaji.

Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 23, 2026, ilihusisha Kiwanda cha SUMAJKT Bottling Company Limited, kinachozalisha maji ya Uhuru Pick, pamoja na Kiwanda cha Ushonaji cha SUMAJKT Garments Co. Ltd, vyote vilivyopo Mgulani.

Kamati hiyo ilipokelewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), aliyeongoza ujumbe wa viongozi waandamizi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata, ameishukuru Kamati kwa ziara hiyo na kusisitiza kuwa shirika litaendelea kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za ushonaji na maji ya Uhuru Pick.

Akihitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Najma Giga, amelipongeza shirika hilo kwa ubunifu na utekelezaji wa majukumu yake, akieleza kuwa Kamati ina imani kubwa na mchango wa SUMAJKT katika uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma nchini.















No comments:

Post a Comment