Na Boniphace John -Dododma
Jeshi la Polisi ,Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma kupitia Kitengo Cha Dawati la Elimu kwa Umma kwa kushirikiana na Chuo cha (WIDE INSTITUTE OF DRIVINGI) kilichopo Dodoma limefanya kampeni ya kutoa elimu ya usalama barabarani katika Soko la Machinga Complex Dodoma, ikiwalenga makundi yote yanayotumia barabara lengo hasa ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na Adha ya changamoto ya ongezeko la ajali Barabarani .
limewakumbusha haki na wajibu wa abiria wanapotumia barabara au wakiwa kwenye chombo cha moto.
Akizungumza wakati wa kampeni hiyo oktoba 31,2026 jijini Dodoma Sajenti Ester Makali amesema elimu hiyo imewalenga watembea kwa miguu, madereva wa daladala, bajaji na bodaboda, kwa lengo la kuwakumbusha matumizi sahihi ya barabara na tafsiri ya alama za barabarani.
Amesema alama za barabarani zimegawanyika katika makundi matano na ni lazima kwa kila mtumiaji wa barabara kuzifahamu ili kuepuka ajali, Jeshi la Polisi limetahadharisha.
Sajenti Ester amewataka abiria kuwa makini zaidi wanapoanza safari, ikiwemo kumtambua dereva pamoja na kondakta wake wa chombo wanachopanda ili iwe rahisi kumbaini pindi tatizo litakapotokea njiani.
amesisisitiza kuwa abiria wana wajibu wa kutoa tahadhari kwa dereva anapokwenda mwendo kasi au anapovunja sheria za barabarani, na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale dereva anapokaidi.
Katika hatua nyingine, Sajenti Makali amewakumbusha abiria kuepuka kupanda magari yasiyoidhinishwa, hususani kwa safari za masafa marefu, kwani magari hayo hayana usajili wala bima ya abiria.
Aidha, amewatahadharisha abiria kutopokea vyakula na vinywaji kutoka kwa watu wasiowafahamu wakiwa safarini.
Akitolea mfano wa matukio ya hivi karibuni ambapo watu waliopokea vyakula njiani walipata madhara makubwa baada ya kutiwa dawa za usingizi na kuporwa mali zao.
Sajenti Makali amesisitiza kuwa usalama barabarani ni jukumu la kila mdau na si la Jeshi la Polisi peke yake, na kuwataka watumiaji wa barabara kutumia vivuko salama wanapotaka kuvuka.
"Unapotumia barabara kumbuka familia yako inakutegemea utarudi salama. Unapaswa kuzingatia sheria za usalama barabarani," ameongeza.
Aidha, ametoa tahadhari kwa madereva na watumiaji wote wa barabara kuchukua tahadhari kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka na msimu wa mvua zinazotarajiwa kuwa juu ya wastani, kwa kuzingatia hali ya hewa kabla ya kutumia barabara.
"Kama hali ya hewa ni ngumu au kuna hatari, usitumie barabara katika wakati huo. Usalama wetu kwanza na usalama wa watumiaji wengine," amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo cha (WIDE INSTITUTE OF DRIVING) Mkufunzi Faustine Matina, amesema kampeni hiyo inalenga kuwajengea uelewa watumiaji wa barabara kuhusu haki na wajibu wao wanapokuwa safarini .
Matina amesema muda wa kampeni hiyo umetelowa kwa wakati sahihi kwani muda mfupi ujao wanafunzi wanatarajia kufunga shule, ambapo familia nyingi husafiri, hivyo ni muhimu wazazi na wanafunzi kuwa na uelewa wa sheria za barabarani.
"Tumeona elimu imetolewa na Jeshi la Polisi kupitia Sajenti Ester ambaye amezungumzia haki na wajibu wa abiria wanapotumia barabara au wakiwa kwenye chombo cha moto. Tunaamini wananchi watakuwa salama hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambacho huwa kuna dhana kuwa ajali huwa ni nyingi," alisema Matina.
Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza chuoni hapo kupata mafunzo stahiki ya udereva ili kuwa madereva wazuri na kupata nyaraka zinazotambulika kisheria kwa utaratibu rafiki.





No comments:
Post a Comment