NEMC, TNBC NA TPSF ZAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA HUDUMA ZA EIA KWA WAWEKEZAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 20, 2026

NEMC, TNBC NA TPSF ZAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA HUDUMA ZA EIA KWA WAWEKEZAJI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na Kiongozi wa Tanzania National Business Council (TNBC) pamoja na Rais wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) kujadili namna ya kutatua changamoto za masuala ya mchakato wa tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (EIA) na upatikanaji wa vyeti.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao waliwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji nchini katika sekta ya Mazingira.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi ameelekeza watumishi wote kuhakikisha masuala ya EIA yanashughulikiwa kwa wakati, wawekezaji wanahudumiwa kwa heshima na malalamiko yanapatiwa ufumbuzi, huku akiitaka Kurugenzi ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Mameneja wa Kanda kusimamia kikamilifu utendaji wa watumishi walio chini yao.

Aidha, amesisitiza kuwa NEMC itaendelea kutekeleza jukumu lake la kulinda mazingira na kusimamia maendeleo endelevu kwa kuzingatia sheria, bila kuwakwaza wawekezaji wanaofuata taratibu, huku ikihakikisha huduma zinatolewa kwa haki, uwazi na ufanisi.

No comments:

Post a Comment