LADIES FIRST KUWA MKAKATI WA BMT KUINUA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MICHEZO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 28, 2026

LADIES FIRST KUWA MKAKATI WA BMT KUINUA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MICHEZO



Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msitha, amesema mashindano ya riadha ya wanawake ya Ladies First ni sehemu ya mipango mkakati ya BMT inayolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika michezo, kutambua vipaji vilivyopo na kuibua vipaji vipya.



Amesema BMT inalenga kuhakikisha wasichana na wanawake wanapata fursa na mazingira wezeshi ya kushiriki michezo, kuendeleza uwezo wao na kufikia mafanikio katika ngazi mbalimbali za ushindani.

Bi. Msitha ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Ladies First yanayofanyika Novemba 28 hadi 29, 2026, Kibaha mkoani Pwani, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa fursa kwa wanawake kuonesha uwezo wao na kujenga mustakabali wa michezo nchini.


No comments:

Post a Comment