MADEREVA WATAKIWA KUSOMA BARABARA KUEPUKA AJALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 29, 2026

MADEREVA WATAKIWA KUSOMA BARABARA KUEPUKA AJALI


Madereva nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kusoma na kutafsiri alama, ishara pamoja na mazingira ya barabarani wanapokuwa wakiendesha vyombo vya moto hatua inayotajwa kuwa muhimu katika kutambua hatari mapema na kuepusha ajali.


Hayo yameelezwa na Sajenti Ester Makali kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Dawati la Elimu kwa Umma Mkoa wa Dodoma mara baada ya kutoa elimu kwa wanafunzi wanaosoma udereva katika moja ya chuo kinachotoa elimu hiyo kilichoko mkoani humo.


Amesema barabara hutoa taarifa mbalimbali kupitia alama, tahadhari na ishara ambazo dereva anapaswa kuzitambua na kuzifanyia kazi ili kuzuia ajali.


"Dereva anapaswa kuwa makini kwa kutazama mbele na pembezoni mwa barabara, kutambua hatari zinazoweza kujitokeza, kuacha nafasi salama kati ya gari lake na gari la mbele pamoja na kutoa kipaumbele kwa vyombo vya dharura,"amesema.


Amesema elimu ya udereva inapaswa kumjengea dereva uwezo wa kujihami dhidi ya hatari, si kuendesha chombo cha moto pekee huku akiwahimiza madereva kujifunza na kubadilika kutokana na makosa yanayoweza kuhatarisha usalama barabarani.


Aidha, amewahimiza vijana wanaotaka kuingia katika taaluma ya udereva pamoja na madereva waliopo tayari barabarani kutafuta elimu sahihi, kuwa tayari kujifunza na kubadilika ili kupunguza makosa yanayochangia ajali za barabarani.


"Uelewa wa kutosha wa sheria, kanuni na mbinu za usalama barabarani ni msingi wa kuwa dereva bora na kulinda maisha ya watumiaji wote wa barabara,"amesema.

No comments:

Post a Comment