![]() |
Meneja Utetezi TWAWEZA Annastazia Rugaba akizungumza katika Sherehe ya kuwatunuku walimu mahiri bakshishi ya KIUFUNZA awamu ya tatu (2019-2021) unaoratibiwa na TWAWEZA may 7,2022. (PICHA NA TWAWEZA) |
Na Okuly Julius Dodoma
Amesema hayo May 7,2022 Jijini Dodoma wakati akifungua Sherehe ya kuwatunuku walimu mahiri bakshishi ya KIUFUNZA mpango wa tatu (2019-2021) iliyoandaliwa na TWAWEZA kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya ofisi ya Rais TAMISEMI .
Prof.Mkenda amesema kuwa ukiwa na walimu wenye ubora ni lazima elimu itakuwa bora hivyo amewapongeza TWAWEZA kwa kuja na mradi huu wa KIUFUNZA ambapo itachochea kila mwalimu kuongeza ubunifu katika kazi yake awapo darasani na matokeo yake itasababisha elimu yetu kuendelea kuwa bora zaidi.
"Niwapongeze sana TWAWEZA chini ya Mkurugenzi wake AIDAN EYAKUZA kwa ubunifu huu kwa sababu matarajio yetu kama Wizara ni kuweka alama katika serikali hii Awamu hii ya sita chini ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan hivyo TWAWEZA mnatuonesha njia kwa vitendo," Prof.Mkenda
Katika kuhakikisha maboresho ya Elimu yanafanyika Prof.Mkenda amesema kuwa kwa sasa wizara inaendelea kupitia baadhi ya Sera,Sheria na Mitaala iliyopo hivyo ikiwezekana kupunguza au kuongeza mambo muhimu ili kufanya elimu yetu iendelee kuwa bora zaidi ikiwemo pia kuhakikisha kuna kuwepo na mazingira salama ya kujifunzia na kufundishia (Miundombinu na Vitendea kazi) ambapo kwa hapa Serikali imeshapiga hatua kubwa sana.
"Agenda yetu ya sasa ni kuhakikisha Sera,Sheria ,Mitaala, Miondombinu pamoja na vitendeaKazi vinaboreshwa ili kuhakisha huu wimbo wa kuwa na Elimu bora unakamilika kwa viwango vinavyotakiwa." Amesema Prof.Mkenda
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa ubora wa elimu unakuwepo nchini wameandaa mkutano wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki mwishoni mwa mwezi Juni na mawaziri wa elimu na wataalamu wa sekta ya elimu kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Ureno,Pakistan, South Africa, Kenya,Sierra Leone wenye lengo la kuzungumzia ubora wa elimu na kupata uzoefu wa mataifa mengine katika sekta ya elimu.
Pamoja na Mkutano huo Prof.Mkenda ameongeza kuwa Mwezi wa Tisa pia kutakuwepo na Mkutano wa wakuu wa nchi la kimataifa la Elimu kujadili Mageuzi ya Elimu Duniani hivyo anaamini kupitia Mkutano huo watapata uzoefu wa kutosha ili kuendelea kuboresha Elimu nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TWAWEZA AIDAN EYAKUZA amesema kuwa kwa sasa TWAWEZA baada ya kukamilisha mradi huu wa awamunya tatu wa KIUFUNZA kwa kushirikisha shule 100 nchini wana mpango wa kuongeza idadi ya shule hadi kufikia 300 na mikoa 10 katika wilaya 30 hapa nchini ila kupanua wigo wa mradi huu.
EYAKUZA ameongeza kuwa kuwapa walibu Bakshishi inawasaidia sana kuhamasika na kubuni mbinu mbalimbali za kufundisha wanafunzi kwa kuzingatia KKK hivyo kuongeza ubora wa elimu nchini kwani lengo la mradi huu ni kuwafanya wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu kuwa na uwezo wa kusoma,kuandika na kuhesabu.
"KIUFUNZA awamu ya tatu imesaidia sana walimu na wanafunzi kwa sababu kiwango cha elimu kimepanda hasa katika shule zote ambazo mradi huu umepitia hivyo nawaomba serikali kuwapatia motisha walimu ili wafanye kazi kwa ubunifu mkubwa huku wakiamini kuwa mwisho wa mwaka kuna Bakshishi atapokea kama motisha hiyo itafanya kiwango cha elimu kukuwa zaidi"Amesema EYAKUZA
Naye Mratibu wa KIUFUNZA MICHAEL KAMUKULU amesema kuwa katika kujenga nyumba ni lazima uanzie kwenye msingi na sio kwenye kuezeka ndio maana wao kama TWAWEZA wakaja na mradi huu ambao umejikita katika madarasa ya chini kabisa la 1,2 na 3 ili kumjengea mwanafunzi msingi mzuri.
Mikoa ambayo imefanikiwa kupitiwa na mradi huo wa KIUFUNZA ni Kigoma,Tanga,Singida,Songwe na Pwani ambapo imekuwa wanufaika wa mpango wa tatu wa KIUFUNZA unaoratibiwa na TWAWEZA.
No comments:
Post a Comment