Na. Asila Twaha, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amewataka Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa kutokukwepa majukumu yao kwa kuwa wao ni sehemu ya Serikali na wanapaswa kujua nafasi walionayo katika maneo wanayotoa huduma.
Ameyasema hayo leo wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Maafisa Watendaji wa Kata na Tarafa wa Mkoa wa Singida kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ambapo mafunzo hayo yanalengo la kuwakumbusha utekelezaji wa majukumu yao kwenye maeneo yao.
Amekemea tabia ya baadhi ya maafisa hukwepa majukumu yao na kuchagua kazi za kufanya na wakati mwengine kutoa lawama kwa Serikali huku wakisahau kuwa wao ndio wawakilishi wa Serikali na wamewekwa hapo ili kuwahudumia wananchi .
“mnajisahau kuwa nyie ndio Serikali wa eneo husika mnalofanyia kazi mnapaswa kushughulikia kila sekta kama elimu, miundombinu, afya, kilimo,uvuvi, amani, usalama, michezo na maafa yote haya mnapaswa kushughulika nayo"
Mhandisi Muragili amewataka maafisa hao pindi mafunzo yatakapomalizika watakuwa wamejifunza na kuenda kufanyia kazi kwa kufanya maamuzi kipi wanapaswa kushughulikia katika ngazi zao.
Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais- TAMISEMI Hamisi Mkunga amewakumbusha maafisa hao kuenda kuyafanyia kazi yale yote waliofundishwa kwa kuwa mada zilizofundishwa zinaenda sambamba na utekelezaji wa majukumu yao hivyo hakutakuwa na kisingizio cha kutokufanya kazi kwa sababu ya kutokujua Sheria, Taratibu na Kanuni na miongozo.
“mafunzo haya mliopatiwa mkatekeleze kwa vitendo tutawapima” amesisitiza Mkunga
No comments:
Post a Comment