NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Zainab Katimba amesema katika mwaka wa fedha 2023/24 Serikali ilitenga Sh Bilioni 2.64 kwa ajili ya kugharamia taulo za kike ambapo kati ya fedha hizo Sh bilioni 1.06 ni za ruzuku ya uendeshaji na Sh bilioni 1.58 ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mhe Katimba ameyasema hayo bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Nora Mzeru aliyehoji nini mpango wa serikali kutenga bajeti kwa ajili ya taulo za kike mashuleni.
Amesema hadi kufikia Machi, 2024 Sh Bilioni 2.2 zimetumika ambapo pia wadau mbalimbali walichangia jumla ya Sh bilioni 1.5 na miradi ya shule ya elimu ya kujitegemea ilichangia Sh milioni 119.5.
Mhe Katimba amezisisitiza Halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili ya upatikanaji wa taulo za kike shuleni
No comments:
Post a Comment