TEWW yamlilia Lugakingira - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 2, 2024

TEWW yamlilia Lugakingira

Prof. Ng'umbi (Mwenye shati jeupe) na baadhi ya watumishi wa TEWW wakiwa wenye nyuso za simanzi wakati wa ibada ya kumwombea Marehemu Lugakingira leo Oktoba 2, 2024 jijini Dar es Salaam.
Bibi Mary Watugulu akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya TEWW mara baada ya ibada ya kumwombea Marehemu Lugakingira leo Oktoba 2, 2024.
Prof. Ng'umbi akibadilishana mawazo na Mkuu wa TEWW mstaafu, Bibi Lambetha Mahai walipokutana katika msiba wa Marehemu Lugakingira leo Oktoba 2, 2024.

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam 


LEO Oktoba 2, 2024 Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Michael Ng'umbi amewaongoza watumishi wa TEWW kuomboleza na kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa TEWW, Mipango, Utawala na Fedha, Marehemu Edward Rwebugisa Lugakingira.

Mzee Lugakingira alifariki Septemba 29, 2024 Hospitali ya Taifa ya Rufaa Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya TEWW, Bibi Mary Watugulu, ameeleza kuwa Marehemu Lugakingira alifanyakazi TEWW kwa zaidi ya miaka 30 na kutoa mchango mkubwa  katika maendeleo ya Taasisi.

Mwili wa Marehemu utasafirishwa kwa ndege leo kuelekea mkoani Kagera kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa kijijini Buganda, Tarafa ya Kamachumu wilayani Muleba.

Takribani watumishi 50 wa TEWW kutoka Makao Makuu, Kampasi ya Dar es Salaam, Kampasi ya Morogoro, pamoja na baadhi ya watumishi wastaafu wamehudhuria ibada ya kumwombea Marehemu  iliyofanyika nyumbani kwake Majumba Sita, Ukonga na kutoa heshima zao za mwisho.

No comments:

Post a Comment