OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema serikali kupitia Halmashauri za mkoa wa Mwanza inaendelea kutekeleza jukumu la utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake waliokidhi vigezo kwa kuzingatia Sheria, taratibu na miongozo ya utoaji na usimamizi wa mikopo ya mwaka 2024.
Mhe. Katimba ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalum Mhe. Kabula Enock Shitobela, aliyetaka kujua
“Je,ni sababu gani zinapelekea kuchelewa kutolewa kwa mikopo ya wanawake waliokidhi vigezo vyote hasa wanawake wa Mkoa wa Mwanza.”
“Serikali kupitia Halmashauri za mkoa wa Mwanza inaendelea kutekeleza jukumu la utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake waliokidhi vigezo kwa kuzingatia Sheria na kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo za mwaka 2024.
Mikopo hiyo hutolewa kwa utaratibu mahususi unaolenga kuhakikisha uwazi, usawa na ufanisi katika usimamizi wa fedha hizo.” amesema
Amesema kwa mujibu wa kanuni hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa hushughulikia maombi ya mikopo yanayowasilishwa katika ngazi ya kata na kufuata hatua muhimu ikiwemo uchambuzi wa vikundi, ukaguzi wa miradi, tathmini ya maombi, uhakiki wa taarifa na utoaji wa mafunzo.
Mhe. Katimba ameongeza kuwa, mchakato huo unatekelezwa ndani ya siku 60 tangu tarehe ya mwisho ya kupokea maombi, ambayo hupokelewa ndani ya siku 30 baada ya kutolewa kwa tangazo. Hali hii husababisha kuchelewa kwa utoaji wa mikopo, si kwa nia ya kuwanyima fursa wanawake bali kwa madhumuni ya kuhakikisha utaratibu wa utoaji wa fedha hizi hunafanywa kwa usahihi na kwa vikundi vilivyo tayari kutekeleza miradi kwa ufanisi.
Serikali inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kwa kutambua hilo, imeendelea kutoa elimu, kuimarisha mifumo na taratibu za utoaji mikopo ili kupunguza ucheleweshaji usio wa lazima.

No comments:
Post a Comment