DKT. JINGU ATAKA ELIMU YA STADI YA MAISHA IGUSE JAMII - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 4, 2025

DKT. JINGU ATAKA ELIMU YA STADI YA MAISHA IGUSE JAMII



WMJJWM- Dodoma


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu, ametaka huduma na elimu ya stadi za maisha zinazotolewa katika Makao ya Taifa ya kulelea watoto Kikombo Dodoma kufikia Jamii.

Dkt. Jingu amesema hayo Juni 03, 2025, baada ya kufanya ziara ya kutembelea Makao hayo kwa lengo la kukagua miradi na huduma zinazotolewa ikiwemo mafunzo ya kushona, kilimo na ufugaji wa samaki.

"Kwa sababu miradi hii inawajengea uwezo watoto wetu wanaolelewa hapa na ndio lengo la Wizara kwamba wapate maarifa wayatumie kujipatia maendeleo wanapotoka hapa ni wakati sasa huduma hizi zikawafikia pia watoto ambao wanaishi katika maeneo Jirani kwa namna hiyo tutakuwa tunasaidia Jamii kujipatia Maendeleo na kuongeza nguvu kazi yenye tija katika Taifa" amesema Dkt. Jingu.

Aidha, Dkt. Jingu amewapongeza watumishi Kikombo kwa kazi nzuri ya kulea na kuhudumia watoto na kuwaomba kuendelea na moyo wa kujitolea kusaidia watoto hao.

Dkt. Jingu akiwa amembatana na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando pamoja na Kamishna Msaidizi Faithmary Lukindo, wametembelea Mradi wa uzalishaji samaki, kilimo cha nyanya, kilimo cha papai, zahanati, Shule na Karakana ushonaji nguo.

Awali akiwasiliaha taarifa ya Maendeleo ya miradi, Mfawidhi wa Makao hayo Jonas Tarimo amesema watoto wanaendelea kupata huduma stahiki, kama chakula, elimu, afya jambo linalowafanya kujifunza na kufanya vizuri katika masomo yao.

Tarimo ameishukuru Wizara kwa kuendelea kutoa mahitaji na huduma mbalimbali kwa watoto wanaoelelewa katika Makao hayo, jambo linalowapa faraja na amani kulelewa hapo.









No comments:

Post a Comment