WAZIRI MKUU AMEONGOZA KIKAO CHA KUMI NA TATU CHA KAMATI KUU YA TAIFA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 25, 2025

WAZIRI MKUU AMEONGOZA KIKAO CHA KUMI NA TATU CHA KAMATI KUU YA TAIFA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022




NA. MWANDISHI WETU


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ameongoza kikao cha Kumi na Tatu cha kamati hiyo kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2025 katika ukumbi wa Kambarage Hazina Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimeudhuriwa na Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara za Kisekta, Makamisaa wa Sensa pamoja na baadhi ya wakuu wa Taasisi.Lengo la kikao hicho ni kupokea na kujadili ripoti mbalimbali za utekelezaji wa Awamu ya Tatu na ya Mwisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Aidha miongoni mwa ripoti hizo ni pamoja na ile ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa kipindi cha kuanzia Desemba 2024 hadi Mei 2025, na Hali ya Utekelezaji wa Anwani za Makazi.

Pia kikao kimejadili na kupokea Rasimu za Ripoti Tano za kina za Matokeo ya Sensa, na Ripoti ya Makadirio ya Idadi ya Watu kuanzia mwaka 2023 hadi 2050 ngazi ya Mikoa.









No comments:

Post a Comment