MIGOGORO MBALIMBALI KUTATULIWA NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KATIKA MAONESHO YA NANENANE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 7, 2025

MIGOGORO MBALIMBALI KUTATULIWA NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KATIKA MAONESHO YA NANENANE



Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amesema kuwa uwepo wa Wizara ya Katiba na Sheria katika maonesho na Sikukuu ya Wakulima kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma utawezesha kupunguza migogoro ya ardhi

Shekimweri ameongeza kuwa utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia unaofanyika katika banda la Wizara hiyo utasaidia kupunguza migogoro hususan ya ardhi ambayo bado ni mingi mkoani hapo.

Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwani wizara hiyo inashughulika na kusikiliza kero, malalamiko na changamoto mbalimbali hivyo basi wananchi watumie fursa hii kuiwasilisha na waweze kupata ufumbuzi kutoka kwa wataalamu wa kisheria.

"Nimefurahi sana kukuta banda la Wizara ya Katiba na Sheria linatoa huduma hii ya Msaada wa kisheria lakini pia inatoa elimu hivyo nawaasa sana wananchi wote wafike hapa kupata elimu na huduma ya utatuzi wa migogoro pia kinamama mjitokeza kwa wingi kujifunza hususan Masuala ya mirathi kwani wengi ndio wahanga wa masuala hayo", amesema.

Aidha Shekimweri amepongeza huduma ya elimu na utawala bora inayotolewa kwani itawafaa wananchi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

"Tunaelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu kwahiyo wananchi wanaofika katika banda hili wananufaika na elimu hii itakayowasaidia kutambua wajibu na haki zao ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo," amesisitiza Shekimweri.











No comments:

Post a Comment