WADAU WAASWA KUUNGANISHA NGUVU UTEKELEZAJI AGENDA YA WANAWAKE, AMANI NA USALAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 18, 2025

WADAU WAASWA KUUNGANISHA NGUVU UTEKELEZAJI AGENDA YA WANAWAKE, AMANI NA USALAMA



Na WMJJWM- Dar Es Salaam


Wadau mbalimbali wameaswa kuunganisha nguvu na kushirikiana katika kuhakikisha utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029 inafikia malengo yaliyokusudiwa ili kuondoa vikwazo vyote vinavyowazuia wanawake kushiriki kikamilifu katika masuala ya amani na usalama.

Hayo yamesemwa mkoani Dar Es Salaam Agosti 18, 2025 na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu
wakati wa akifungua Kongamano kuelekea Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029.

Dkt. Jingu amesema ni muhimu kuimarisha elimu na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa usawa wa kijinsia kama msingi wa amani endelevu, sambamba na kuweka mifumo thabiti ya ufuatiliaji na tathmini ili kuhakikisha kuwa hatua zinazochukuliwa zinafanikiwa na zinaendana na malengo ya Mpango Kazi huo.

"Kwa kufuata mwelekeo huu, Tanzania itaendelea kujenga hadhi yake kama mfano wa kuigwa, ikithibitisha kuwa ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama si ndoto bali ni hatua halisi za maendeleo, usawa na ustawi wa kijamii." amesema Dkt. Jingu

Kwa upande wake Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UN Women Katherine Gifford, amesema Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029 ni mwelekeo mzuri katika kuhakikisha Mwanamke anashirikishwa katika masuala ya amani na usalama hivyo Mpango huo unapaswa kuwekwa katika utekelezaji zaidi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Brigedia Jenerali George Itang'are ameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kuandaa Mpango Kazi huo ambao ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ya kuhakikisha Mwanamke anashirikishwa katika masuala muhimu ya amani na usalama.






No comments:

Post a Comment