
Septemba 25, 2025 Mahakama ya Wilaya ya Morogoro mbele ya Hakimu Mh. V. Kitauka katika shauri la Rushwa namba 23268/2025 imemtia hatiani Askari mhifadhi wa Hifadhi ya Asili ya Mlima Uluguru Bw. BERNARD MWAITUKA kwa kujipatia fedha kwa njia ya Rushwa kiasi cha shilingi 450,000/= ili aweze kuachilia mbao na mashine za kukatia mbao (chain saw) alizokua amezikamata na kuzishikiilia kwamba hazina vibali halali.
Mshtakiwa huyo alikuwa anakabiliwa na Shtaka la Rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a)&(2) PCCA R.E 2023.
Baada ya Mshtakiwa kutiwa hatiani ametakiwa kulipa faini ya Tsh 500,000/= au kwenda Jela miaka 3. Na kutakiwa kurejesha jumla ya kiasi cha 450,000/= alizokuwa amejipatia.
Mshtakiwa amelipa faini ili kuepuka kifungo na pia amerejesha kiasi cha Tsh 450,000/= alichojipatia kwa njia ya hongo.
Shauri hili liliendeshwa na waendesha mashtaka wa TAKUKURU Bi.Husna kiboko na Bi.Felister Chamba.
TAKUKURU (M) MOROGORO SEPTEMBA, 26, 2025
No comments:
Post a Comment