
MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewahutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani.
Dk.Nchimbi ametoa ombi hilo leo Septemba 3,2025 alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara ambapo katika mkutano huo amewanadi Wabunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.
Wengine ni Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu, Lucy Mayenga , Jimbo la Solwa Ahmed na Itwangi na Azza Hillal pamoja na madiwani.
Dkt. Nchimbi ameendelea kunadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Aidha amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025








No comments:
Post a Comment