
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria kwenye Mkutano wa Kampeni za CCM Nungwi, Kaskazini Unguja leo Alhamisi Septemba 18, 2025. Katika hotuba yake Dkt. Samia ameahidi kuendelea kukuza uchumi na kipato cha mwananchi kwa kuendelea kubuni na kusimamia mikakati yake ya kuzalisha fursa za ajira, utoaji wa mikopo, urasimishaji pamoja na elimu ya ujuzi kwa Vijana ili kuweza kuwa na shughuli za kiuchumi na uzalishaji.






No comments:
Post a Comment