UCHUMI WA TANZANIA BARA UTAKUA KWA ASILIMIA 7 MWAKA 2026/27- DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 18, 2025

UCHUMI WA TANZANIA BARA UTAKUA KWA ASILIMIA 7 MWAKA 2026/27- DKT. SAMIA



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ikiwa Watanzania watampa ridhaa ya kuongoza serikali kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Ukuaji wa Uchumi kwa Tanzania bara utafikia asilimia saba kwa mwaka kufikia mwaka wa fedha 2026/27.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 18, 2025 kwenye siku yake ya pili ya Kampeni Visiwani Zanzibar huko Nungwi, Kaskazini Unguja, amewaambia washiriki wa Mkutano wake wa kampeni kuwa hilo litawezekana kama ilivyo Zanzibar kutokana na ushirikiano uliopo katika utekelezaji wa sera za uchumi na fedha kwa pande zote mbili za muungano.

"Sera za kiuchumi na kifedha zimefanya kazi nzuri zaidi na tumeweza kukua. Tulikuwa tunakuwa kwa asilimia 7 kabla ya Covid na kuporomoka kwa uchumi lakini Dkt. Mwinyi ameweza kurudi haraka kwenye asilimia saba, nasi tuna matumaini mwakani 2026/27 tutarudi kwenye asilimia 7 kama ilivyo Zanzibar." Amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia amesema uchumi kwa Tanzania bara na Zanzibar uliyumba zaidi mwaka 2020 kutokana na janga la Uviko-19, kuporomoka kwa uchumi wa dunia pamoja na kupungua kwa misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo kabla ya jitihada kubwa kufanywa na serikali mbili za Muungano na hivyo kuweza kuhimili misukosuko ya kiuchumi iliyokuwepo.

Amesema baada ya utekelezaji wa mikakati na sera mbalimbali, serikali zote mbili (ile ya Muungano na ya Zanzibar) zimefanikiwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta za afya, elimu, maji na miundombinu huku pia akikiri kuwa ukuaji huo wa uchumi umemgusa pia mwananchi mmoja mmoja suala ambalo linaonekana dhahiri kupitia ustawi na maendeleo ya Kaya za Nungwi na maeneo mengine nchini.






No comments:

Post a Comment