DKT. SAMIA KUANZA KAMPENI ZAKE MKOANI PWANI LEO SEPTEMBA 28. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 28, 2025

DKT. SAMIA KUANZA KAMPENI ZAKE MKOANI PWANI LEO SEPTEMBA 28.



Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Septemba 28, 2025 anatarajiwa kuendelea na kampeni zake Mkoani Pwani ili kunadi Ilani ya CCM ya 2025/30 pamoja na kuomba kura kwa wananchi wa Mkoa huo.

Dkt. Samia ambaye ametokea mikoa ya Kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma anatarajiwa leo kuanzia Kampeni zake kwenye Wilaya za Kibaha, Chalinze na baadaye Msata, akifanya mikutano mikubwa ya kampeni kwenye maeneo hayo kabla ya kuelekea kwenye Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo Tanga na Arusha.

Akiwa Mtwara Mjini kwenye Mkutano wake wa kuhitimisha Kampeni Mkoani Mtwara, Dkt. Samia ameahidi kuimarisha kilimo cha Korosho mkoani humo, akiahidi kuweka jitihada zaidi katika upatikanaji wa pembejeo na huduma za ugani ili kuiwezesha Tanzania kuendelea kuwa mzalishaji mkubwa wa zao hilo la biashara, akiahidi pia kuiunganisha Mtwara na njia zote za usafiri na usafirishaji ikiwemo ujenzi wa reli kutoka Mtwara kwenda Mbamba Bay ili kurahisisha biashara kati ya Mkoa huo na nchi za Msumbiji na Malawi.

Dkt. Samia kadhalika ameahidi kuendelea kutafuta masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo ikiwemo Korosho, mbaazi na ufuta, kukamilisha mradi wa umeme utakaounganisha mikoa ya Mtwara na Lindi kwenye gridi ya Taifa pamoja na ujenzi wa vituo vya kupooza umeme ili kuhakikisha mikoa hiyo inaondokana na tatizo la umeme hafifu na kutokuwa wa uhakika sambamba na kuwekeza katika matumizi makubwa zaidi ya teknolojia katika sekta mbalimbali pamoja na kuchukua hatua zaidi katika kulinda mila na desturi za Mtanzania.

No comments:

Post a Comment