MAENDELEO BUKOMBE YAWANG’ARISHA SAMIA NA BITEKO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 13, 2025

MAENDELEO BUKOMBE YAWANG’ARISHA SAMIA NA BITEKO



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitano imetekeleza miradi mingi ya maendeleo ambayo imeboresha maisha ya wananchi.

Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 12, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Bukombe wilayani Bukombe mkoani Geita, ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

“ Tunafanya kazi ya kuleta maendeleo uchaguzi wa mwaka huu umegawanyika mara mbili wapo wanaozungumzia matamanio na sisi tunaosema tuliyoyatekeleza,” amesema Dkt. Biteko

Ameongeza “ Kata ya Bukombe tunafahamu sasa tunajenga madarasa manne Imaranguzu, miaka mitano iliyopita tulikuwa na shule chache sana tukaona tujenge maeneo ambayo hayakuwa na shule na tumeanza kukarabati shule kongwe,”

Amesema licha ya kuwa na Zahanati ya Bukombe ambayo inaendelea kutoa huduma kwa watu wengi, sasa kuna mpango wa kuipandisha hadhi kuwa kituo cha afya.

Amesema mipango mingine ya maendeleo katika Kata hiyo ni ujenzi wa mradi mkubwa wa maji ambao utatekelezwa katika kipindi cha mwaka 2025-2030.

Amesema hadi kufikia Desemba mwaka huu Serikali ya CCM itahakikisha inapeleka umeme katika maeneo yaliyobaki katika Jimbo lake pamoja na kufunga taa za barabarani ili vijana na wanawake waweze kufanya biashara.

Kufuatia maendeleo hayo amewahimiza wananchi wa Bukombe kumchagua mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan Oktoba 29 mwaka huu.

Dkt. Biteko amesisitiza “ Hapa kuna wapiga kura 11,000 waliojiandikisha nawaomba wote tukapige kura,”

Naye, Mgombea wa Udiwani Kata ya Bukombe, Rosaria Masokola amesema kuwa Kata hiyo yenye vijiji saba katika kipindi cha miaka mitano imepata fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba ya walimu kwa gharama ya shilingi milioni 63, ujenzi wa zahanati mpya ambayo inatarajiwa kukamilika Novemba mwaka huu.

Ameongeza kuwa Kata hiyo ina zahanati Iliyo kamilika kwa sh milioni 75 na watu wanatibiwa, kuna shule Imaranguzu pamoja na Kidete ambazo wanafunzi wanasoma.

“ Tuna mradi wa maji wa wenye gharama ya sh milioni 500 uliokamilika, barabara imekamikika kwa kiwango cha moramu kutoka Bukombe - Imaranguzu -Karanga, kwa miradi yote hii naomba Oktoba 29 mwaka huu tukapige kura kuwachagua wagombea wote wa CCM,” amesema Masokola.

No comments:

Post a Comment