MAJIKO BANIFU TEKNOLOJIA YA KISASA INAYOTUMIA MKAA KIDOGO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 22, 2025

MAJIKO BANIFU TEKNOLOJIA YA KISASA INAYOTUMIA MKAA KIDOGO



Na Mwandishi Wetu, Geita

Imeelezwa kuwa majiko banifu yanayotolewa kwa bei ya ruzuku na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni majiko yanayotumia kiasi kidogo cha mkaa kulinganisha na majiko mengine ya mkaa.

Hayo yamebainishwa na Wataalam kutoka REA wanaoendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita.

Aidha, majiko banifu yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kupunguza sumu ya mkaa (carbon monoxide) hivyo inasaidia kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na nishati ya mkaa.

Halikadhalika, majiko banifu yanasaidia utunzaji wa mazingira, ni rahisi kwa matumizi yanadumu kwa muda mrefu bila kupata changamoto ya kuharibika kwa watumiaji.

Katika mkoa wa Geita kampuni inayosambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ni Geita Millenium Star Company Limited.

Majiko banifu yanatolewa kwa bei ya ruzuku ya shilingi 6,195 kwa kuwa Serikali imeweka ruzuku ya bei katika majiko hayo ili wananchi waweze kuyatumia na kuyapata kwa urahisi ambapo kabla ya ruzuku yalikuwa yanauzwa kwa shilingi 41,300.



No comments:

Post a Comment