Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Map Mastar MKM wakishirikiana na Nobe wametambulisha rasmi wimbo wao mpya uitwao “Kiongozi Bora”, audio rasmi ikiwa imewekwa kupitia mtandao wa YouTube chini ya Misalaba Media.
Wimbo huu unakuja ukiwa na ujumbe mzito wa kijamii unaogusa nafasi na wajibu wa viongozi bora katika maendeleo ya taifa, ambapo wasanii hao wanatumia sanaa yao kueleza matarajio ya wananchi kwa viongozi wanaojali, kusimamia haki na kusogeza huduma karibu na wananchi.
No comments:
Post a Comment