𝗪𝗔𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗪𝗔𝗠𝗘𝗥𝗜𝗗𝗛𝗜𝗞𝗔 𝗡𝗔 𝗨𝗧𝗘𝗡𝗗𝗔𝗝𝗜 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 - 𝗗𝗞𝗧. 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗠𝗕𝗜 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 28, 2025

𝗪𝗔𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗪𝗔𝗠𝗘𝗥𝗜𝗗𝗛𝗜𝗞𝗔 𝗡𝗔 𝗨𝗧𝗘𝗡𝗗𝗔𝗝𝗜 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 - 𝗗𝗞𝗧. 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗠𝗕𝗜


"Nakushukuru sana Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama chetu cha CCM kwa imani yako kubwa kwangu kwa kunipendekeza kuwa msaidizi wako mkuu, miaka minne iliyopita uliniteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misiri, badae ukanipendekeza kupitia vikao vya Halmshauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Katibu Mkuu wa CCM na sasa umeniamini katika nafasi ya Mgombea Mwenza"

"ndani ya miaka minne umeonesha imani yako kwangu kwa kunipa nafasi muhimu ndani ya Taifa letu na ndani ya CCM"

"nakuhakikishia kuwa imani uliyoonesha, namna pekee ninayoweza kuilipa ni kukusaidia kwa nguvu, akili, maarifa na uaminifu ili ndoto na maono yako na utekelezaji wa ilani yetu ya CCM (2025/30) ufanyike kwa mafanikio makubwa katika miaka mitano ijayo."

"Watanzania katika sehemu zote tulizopita wameridhika na utekelezaji wako wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 kwa kishindo na wametutuma tukueleze kuwa kesho watakupa kura nyingi za ushindi wa kishindo"

"hilo linatokana na utendaji kazi wako katika Serikali ya awamia ya sita unayoiongoza inayotakana na Chama Cha Mapinduzi (CCM)"

Hayo yamesemwa na Mgombea mweza wa Urais katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Ndugu. Dkt. Emmanuel John Nchimbi, wakati akizungumza mbele ya umati wa Wananchi wa Mwanza na maeneo ya karibu katika mkutano wa kuhitimisha Kampeni za Uchaguzi za CCM, leo tarehe 28 Oktoba 2025.





No comments:

Post a Comment