KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KWA USIMAMIZI THABITI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 10, 2026

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KWA USIMAMIZI THABITI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026



Na. Veronica Mwafisi-Dodoma


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Kwa niaba ya Kamati yangu nitoe pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan maana ndiye mwenye ofisi hii, kwa hakika mnafanya kazi nzuri kwa kumwakilisha Mhe. Rais. Amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro

Vilevile, Mhe. Dkt. Ndumbaro amempongeza na kumshukuru Waziri Kikwete kwa taarifa nzuri aliyoiwasilisha kwa Kamati hiyo iliyoelezea kwa kina utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo itaongeza chachu ya maendeleo nchini.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ameiahidi Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kuwa itashirikiana nayo katika usimamizi wa masuala mbalimbali ili kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha kwa mwaka 2025/2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, utekelezaji wa shughuli zilizopangwa katika kipindi husika umefanyika kwa kuzingatia fedha zilizopatikana pamoja na muda wa upatikanaji wake.
Mhe. Kikwete amesema kuwa, lengo la miradi hiyo ni kuongeza tija nchini lakini pia itaongeza chachu ya utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma

Aidha, Mhe. Kikwete ameishukuru na kuiahidi Kamati hiyo kuwa Ofisi anayoisimamia itaendelea kushirikiana nao katika kuimarisha na kuboresha utendaji kazi ili kuleta tija katika kuwahudumia wadau mbalimbali kwa lengo la kujenga na kuimarisha Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.




No comments:

Post a Comment