MAKAMU WA RAIS AZINDUA MFUMO WA KUTABIRI KIASI CHA MAJI KWENYE MITO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, March 22, 2026

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MFUMO WA KUTABIRI KIASI CHA MAJI KWENYE MITO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Emmanuel Nchimbi amezindua Mfumo wa Utabiri wa Kiasi cha Maji kwenye mito nchini Tanzania.

Uzinduzi huo umefanyika katika la Bwawa la Mindu Mjini Morogoro ambako amejionea namna Wizara ya Maji inavyoshiriki katika utunzaji, ulinzi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmasi amesema mfumo huo ni Moja ya jitihada za Wizara ya Maji kuhakikishia inaondoa changamoto za Sekta kwa kuwezesha upatikanani wa taarifa sahihi za kiwango cha Maji.


Amesema Bwawa Hilo ni sehemu ya maeneo yatakayonufaika na changamoto hiyo kwani linapokea maji kutoka sehemu mbalimbali za nchi na linachangia kwa zaidi ya asilimia 70 ya huduma ya Majisafi katika mji wa Morogoro.

Pamoja na uzinduzi wa Mfumo Mhe Nchimbi amepanda miti rafiki wa Maji kwenye chanzo hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani na kilele cha Wiki ya Maji Tanzania.

No comments:

Post a Comment