PROF. SHEMDOE NA VIONGOZI WA OWM-TAMISEMI WASHIRIKI IBADA YA KUMUAGA MAREHEMU WILLIAM LUKUVI JIJINI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 27, 2026

PROF. SHEMDOE NA VIONGOZI WA OWM-TAMISEMI WASHIRIKI IBADA YA KUMUAGA MAREHEMU WILLIAM LUKUVI JIJINI DODOMA



Na OWM - TAMISEMI, Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, leo Machi 27, 2026 ameshiriki katika ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), marehemu Mhe. William Vangimembe Lukuvi.

Ibada hiyo imefanyika katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na Serikali, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.

Katika tukio hilo, Prof. Shemdoe aliambatana na wasaidizi wake akiwemo Naibu Waziri anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagwila, Naibu Waziri anayeshughulikia Afya, Dkt. Mhe. Jafar Seif, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Bw. Adolf Ndunguru pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bw. Sospeter Mtwale.

Marehemu William Lukuvi ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika Utumishi wa Umma na maendeleo ya taifa kwa ujumla, kutokana na uzoefu wake wa kulitumia taifa katika nafasi mbali mbali za uongozi.







No comments:

Post a Comment