DC SIMANJIRO AONGOZA WARSHA YA WORLD VISION KUIMARISHA HUDUMA KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 27, 2026

DC SIMANJIRO AONGOZA WARSHA YA WORLD VISION KUIMARISHA HUDUMA KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM


Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Raphael Lulandala, Machi 25, 2026 ameongoza warsha iliyoandaliwa na World Vision Tanzania, iliyowakutanisha viongozi mbalimbali pamoja na watoto, wazazi na walezi wa watu wenye ulemavu kutoka kata kadhaa za wilaya hiyo.

Warsha hiyo ilihusisha pia Maafisa Watendaji, wenyeviti na madiwani, ambapo kwa pamoja walipokea wasilisho la utafiti uliofanywa na World Vision Tanzania kuhusu hali ya watu wenye mahitaji maalum na nafasi wanayopewa katika jamii.

Aidha, imeelezwa kuwa huduma za kibingwa zimetolewa ikiwemo upimaji, tiba na utoaji wa rufaa kwa watoto wenye changamoto za uoni, usikivu na ujongeaji.

Watoto hao wameanza kupatiwa matibabu, vifaa vya usaidizi pamoja na huduma za rufaa, zote zikigharamiwa na World Vision Tanzania.
Sambamba na hilo, Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea eneo la Orkesmet na kujionea utoaji wa huduma hizo, pamoja na kupokea maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wake kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Akizungumza na wananchi, amesema huduma hizo zinaendelea kutolewa pia katika Tarafa ya Terat, Oljoro Na. 05, kwa lengo la kuwafikia walengwa wengi zaidi na kuboresha ustawi wa watoto wenye mahitaji maalum katika Wilaya ya Simanjiro.


No comments:

Post a Comment