TUNAHITAJI MATOKEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PAMOJA.DKT JINGU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 27, 2026

TUNAHITAJI MATOKEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PAMOJA.DKT JINGU


Na WMJJWM – Dar Es Salaam


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John amasisizitiza kasi katika utekelezaji wa mradi wa kukuza usawa wa kijinsia pamoja na kuleta matokeo yenye tija kwa jamii.

Dkt. Jingu amesema hayo Machi 27, 2026, Jijini Dar es Salaam wakati akiongoza kikao cha Kamati elekezi ya utekelezaji wa mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania (PAMOJA) kwa lengo la kujadili na kuimarisha uratibu na uendeshaji wa mradi huo.

Dkt. Jingu amesema katika utekelezaji wa mradi huo, kila mmoja ahakikishe anatimiza majukumu yake kwa ufanisi kwa nafasi aliyonayo, ili kuleta matokeo tarajiwa ili hatimaye mradi uache alama chanya kwa jamii.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawaka na Makundi Maalum Victor Nkya amesema mradi huo utawanufanisha wanawake kwa kupitia mikopo ili kuendesha shughuli za kiuchumi na kuongeza kipato cha familia.

“Mradi huu utawafikia wanawake wajasiriamali ili kukuza na kuimaridha Uchumi wa kaya jamii na familia kupitia mikopo yenye masharti nafuu, kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kuipitia vikundi vya wanawake mtaani na sokoni, pamoja na kuimarisha malezi hatimaye kutakuwa na Watoto wenye maadili na wenye kuleta tija katika jamii” amesema Nkya.

Mradi wa PAMOJA unatekeleza kwa Tanzania bara na Zanzibar, ukilenga kuimarisha usawa wa kijinsia, kupunguza na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia, kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake, kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuimarisha malezi nchini.

No comments:

Post a Comment