Na WyEST - Dodoma
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kuimarisha ushirikianobna sekta Binafsi katika kuteleza Sera ya Elimu ma Mafunzo 2024 Toleo la 2023.
Leo Machi 9, 2026 jijini Dodoma imekutana na Wamiliki wa Shule Binafsi kujadili ushirikiano wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kufanikisha utekelezaji wa elimu ya lazima ya miaka 10 na elimu ya Amali.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda amekumbusha wadau hao kuwa msukumo wa kuimarisha ubia huo unatokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye wakati wa uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo alisisitiza matumizi ya mfumo wa PPP kama nyenzo muhimu ya kusukuma mbele mageuzi ya elimu.
Aidha, amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kuongeza fursa za elimu nchini, na kwamba inadhamiria kuendeleza mashirikiano hayo katika kutekeleza mageuzi ya elimu.
Kupitia kikao hicho, wadau wa sekta binafsi wamepongeza jitihada za Wizara kwa kuwa na utayari wa kushirikiana kikamilifu katika mageuzi ya elimu, hususan utekelezaji wa elimu ya lazima ya miaka 10 na elimu ya Amali, ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata fursa sawa ya kujifunza na kupata ujuzi.












No comments:
Post a Comment