
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50, Bw. Alain Ebobisse, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, yanayoendelea jijini humo, ambapo Taasisi ya Africa50 iliihakikisha Tanzania kuwa iko tayari kuwekeza nchini Tanzania kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya gesi na umeme ili kuchochea uchumi wa Taifa Kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50, Bw. Alain Ebobisse (wa tano kulia), Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil (watano kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa nne kushoto) na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Taasisi hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, yanayoendelea jijini humo, ambapo Taasisi ya Africa50 ilihakikisha Tanzania kuwa iko tayari kuwekeza nchini Tanzania kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya gesi na umeme ili kuchochea uchumi wa Taifa Kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto) ukiwa katika kikao na ujumbe kutoka Taasisi ya Africa50 inayojihusisha na uwekezaji katika sekta ya miundombinu ukiongozwa na Afisa Mtendaji wake Mkuu, Bw. Alain Ebobisse, kilichofanyika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, yanayoendelea jijini humo, ambapo Taasisi ya Africa50 ilihakikisha Tanzania kuwa iko tayari kuwekeza nchini Tanzania kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya gesi na umeme ili kuchochea uchumi wa Taifa Kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza wakati wa kikao chake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50 inayojihusisha na uwekezaji katika sekta ya miundombinu, Bw. Alain Ebobisse (hayupo pichani), kilichofanyika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, yanayoendelea jijini humo, ambapo Taasisi ya Africa50 ilihakikisha Tanzania kuwa iko tayari kuwekeza nchini Tanzania kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya gesi na umeme ili kuchochea uchumi wa Taifa Kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C, Marekani)
Na Benny Mwaipaja, Washington DC
Taasisi ya Africa50 inayojihusisha na uwekezaji katika sekta ya miundombinu imesema kuwa iko tayari kuwekeza nchini Tanzania kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya gesi na umeme ili kuchochea uchumi wa Taifa Kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Alain Ebobisse, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Washington D.C nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF.
Bw. Alisema kuwa Taasisi yake ina uzoefu mkubwa wa kuwekeza katika nchi za Afrika katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kwamba Tanzania inayo nafasi kubwa ya kupiga hatua kimaendeleo kwa kuvutia mitaji kutoka nje kupitia uwekezaji ambao Taasisi yake iko tayari kuuweka.
“Taasisi yetu imewekeza kati ya dola milioni 20 hadi 30 katika mradi wa kusambaza gesi jijini Dar es salaam kama mradi wa majaribio lakini tunataka kuwekeza zaidi katika sekta hiyo ya gesi na pia tunataka kuwekeza katika mradi wa kusambaza umeme nchini Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Ugavi wa Umeme-TANESCO’ alisema Bw. Ebobisse.
Alisema kuwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zina rasilimali nyingi zinazoweza kuchachua uchumi wake lakini changamoto kubwa ni namna ya kupata mitaji ama fedha za kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi na kwamba Taasisi yake iko tayari kuwa sehemu ya kutatua changamoto hiyo kwa Tanzania.
“Mwaka huu tumepanga kuwa na Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi yetu ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) nchini Tanzania ambapo tunataka kuonesha mambo tunayoweza kuyatekeleza Kupitia ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma na ni fursa nzuri kwa Tanzania kutumia fursa hiyo pia kuwaeleza wawekezaji tutakao waalika maeneo wanayoweza kuwekeza” Aliongeza Bw. Ebobisse.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), aliikaribisha Taasisi hiyo na wawekezaji wengine kwenda kuwekeza nchini Tanzania na kunufaika na vivutio mbalimbali vinavyotolewa kwa wawekezaji.
Mhe. Balozi Omar alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji ikiwemo kupitia upya mifumo ya kodi na mazingira ya uwekezaji ili kuchochea zaidi upatikanaji wa mitaji kutoka nje.
Alisema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliunda Tume mbili muhimu, moja ya kuangalia mifumo ya kodi iliyowasilisha ripoti yake ikiwa na mapendekezo zaidi ya 280 na Tume nyingine inayo angazia eneo la mazingira ya uwekezaji ambayo inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake hivi karibuni.
“Haya yote yanafanyika kwa nia njema ya kuvutia zaidi uwekezaji na mitaji kutoka nje ya nchi lakini pia kuifanya sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kutekeleza mipango na miradi ya Serikali kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050” alisema Mhe. Balozi Omar.
Alieleza kuwa asilimia 70 ya utekelezaji wa Dira 2050 iliyoweka malengo ya nchi kufikia uchumi wa dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, inatakiwa kutoka katika sekta binafsi na asilimia 30 zinatarajiwa kutoka Serikalini na taasisi zake hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuilea na kuikuza sekta binafsi ili malengo hayo yaweze kutumia.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Afisa Uendeshaji Mkuu wa Africa50, Bi. Tshepidi Moremong na viongozi wengine Waandamizi wa Serikali na Taasisi hiyo ya Africa50.
Africa50 ni Taasisi ya uwekezaji wa miundombinu iliyoanzishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB ii kutatua changamoto za uhaba wa miundombinu inayoweza kuchochea ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama wa Taasisi hiyo katika Bara la Afrika.

No comments:
Post a Comment