MHE. BALOZI OMAR ASHIRIKI MKUTANO WA AfG1 wa IMF - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 16, 2026

MHE. BALOZI OMAR ASHIRIKI MKUTANO WA AfG1 wa IMF


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ambaye pia ni Gavana wa Bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ameshiriki Mkutano wa nchi za Kundi la Kwanza za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency) wa Shirika hilo, uliofanyika katika Ofisi za Shirika hilo jijini Washington D.C, nchini Marekani, akiwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika mikutano inayoendelea ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, jijini humo.

Mkutano huo ulijadili Ripoti ya Muda ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Afrika kwa mwaka 2026, na namna ya Kukabiliana na Changamoto za Sekta ya Nje katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) kwa kutumia Mfumo Jumuishi wa Sera wa IMF (IPF).





No comments:

Post a Comment