DKT.JINGU AFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA NCHI ZA MAZIWA MAKUU KUHUSU AJENDA YA WANAWAKE, AMANI NA USALAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 27, 2026

DKT.JINGU AFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA NCHI ZA MAZIWA MAKUU KUHUSU AJENDA YA WANAWAKE, AMANI NA USALAMA



Na WMMJWM-Dra Es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema Ukanda wa Maziwa Makuu umepiga hatua kubwa tangu kupitishwa kwa Azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la mwaka 2000 ambalo ni kiashiria muhimu cha kuonesha juhudi zetu za kushughulikia masuala ya kijinsia kwa amani na usalama.

Dkt. Jingu ameyasema hayo tarehe 27, Aprill 2026 jijini Dar es Salaam wakati anafungua mkutano wa mafunzo kwa maafisa wanaoratibu utekelezaji wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Viongozi na Wawakilishi wa Sekretarieti ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).

"Migogoro kwenye baadhi ya nchi za Maziwa Makuu imeleta mateso makali hasa kwa wanawake na wasichana kupitia unyanyasaji wa kingono na kijinsia. Iwapo migogoro hiyo haitadhibitiwa ipasavyo, kuna uwezekano wa kuleta madhara makubwa zaidi ", amesema Dkt. Jingu.

ICGR inajumuisha nchi wanachama 12 ikiwamo Tanzania, ambazo zinashirikiana katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kuangazia amani, usalama,utawala na maendeleo.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na na Shirika la ujerumani la Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit.


No comments:

Post a Comment