RC MBONI MHITA AONGOZA TAMASHA LA MWANAMKE CHUMA 2026, ATOA WITO WA WANAWAKE KUINUANA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, April 12, 2026

RC MBONI MHITA AONGOZA TAMASHA LA MWANAMKE CHUMA 2026, ATOA WITO WA WANAWAKE KUINUANA

 


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akikata keki na kuzindua kikundi cha Wanawake Chuma katika Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano -Picha - Malunde


Mamía ya wanawake wamejitokeza kushiriki Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano lililofanyika Aprili 11, 2026 katika Ukumbi wa Malex uliopo Kahama, mkoani Shinyanga, huku wito ukitolewa kwa wanawake kushirikiana na kuinua wenzao ili kufikia mafanikio ya pamoja.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, aliyesisitiza umuhimu wa mshikamano, uthubutu na kujiamini kwa wanawake katika harakati za maendeleo binafsi na ya jamii.

Akizungumza katika tamasha hilo, Mhita amewataka wanawake kuacha hofu ya maneno ya watu na badala yake kuzingatia malengo yao kwa vitendo.

“Mwanamke hakikisha unapambana ili kufikia malengo yako, usiogope kusemwa. Wewe songa mbele kwa sababu uwe mzuri utasemwa, uwe mbaya utasemwa, upendeze utasemwa, usipendeze utasemwa. Kuna watu wamevunjika moyo kwa sababu ya kusemwa, hakikisha kuwa upo na watu sahihi, jiamini, usihangaike na watu wenye kukutisha tamaa. Ili mwanamke uonekane umefanikiwa, lazima uinue wanawake wenzako. Uwe nguzo ya kuwainua wengine,” amesema Mhita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita.

Akifafanua zaidi, Mhita amebainisha kuwa katika dunia ya sasa, mafanikio ya mwanamke yanategemea zaidi uthubutu wa kiuchumi, akisisitiza kuwa, “siri ya mwanamke yoyote ni sasampa (pesa), na habari ya mjini ni pesa, hivyo ni lazima mwanamke uhakikishe unazitafuta na kuzitumia fursa zinazokuwezesha kuinuka kiuchumi.”

Ameongeza kuwa wanawake wanapaswa kujiamini na kutumia kikamilifu fursa zilizowekwa na serikali, ikiwemo mikopo na uwezeshaji katika sekta mbalimbali kama madini, kilimo na viwanda, akibainisha kuwa mazingira rafiki yameboreshwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa kupitia maboresho hayo, wanawake wachimbaji wa madini sasa wanapata mikopo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji, huku sekta ya kilimo ikipewa kipaumbele kwa kuongeza bajeti ili wanawake wanufaike zaidi. 

Aidha, ameeleza kuwa hata katika sekta ya viwanda wanawake wameendelea kunufaika na fursa zilizopo na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Mhita amewapongeza wanawake wa Ushetu kwa jitihada zao katika kusindika na kuongeza thamani ya mazao, akieleza kuwa huo ni mfano bora wa namna wanawake wanavyoweza kutumia fursa za kiuchumi kujiletea maendeleo endelevu.

Pia amegusia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya afya na elimu, akieleza kuwa Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi, huku Mkoa wa Shinyanga ukiwa sasa na shule sita za wasichana, hatua inayochochea upatikanaji wa elimu kwa mtoto wa kike na kumjengea msingi imara wa mafanikio ya baadaye.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Gold FM na mwandaaji wa tamasha hilo, Bi. Neema Mghen, amesema Tamasha la Mwanamke Chuma limeendelea kuwa zaidi ya tukio la kawaida na sasa ni jukwaa muhimu la mabadiliko kwa wanawake.
Neema Mghen

Amesema kupitia tamasha hilo, wanawake wengi wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi, kujitambua, kujiamini na kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi na maamuzi ndani ya familia na jamii.

Kaulimbiu ya mwaka huu, “Nguvu ya Ujasiri,” imelenga kuhamasisha wanawake kusimama bila uoga, kuchukua hatua na kutumia fursa zilizopo kubadilisha maisha yao na ya wengine.

Ametaja mafanikio ya msimu wa tano kuwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kikundi cha Mwanamke Chuma Maendeleo Group kilichozinduliwa rasmi wakati wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2026, kusaidia wanawake wa gereza la Kahama kwa kuwapatia mahitaji muhimu, pamoja na kuendeleza utamaduni wa kutoa tuzo kwa wanawake ili kutambua na kuhamasisha juhudi zao.
Hata hivyo, amebainisha changamoto zinazowakabili wanawake kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji na utaalamu katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini, uwepo wa mikopo yenye riba kubwa na masharti magumu, pamoja na changamoto za pembejeo bora na masoko ya uhakika katika sekta ya kilimo.

“Tunaamini ukimuinua mwanamke, umeinua familia na jamii kwa ujumla. Ujasiri wa mwanamke si kelele bali ni hatua, si maneno bali ni matendo,” amesema Mghen.

Ameongeza kuwa Tamasha la Mwanamke Chuma lina lengo la kukuza uchumi wa wanawake mmoja mmoja na vikundi, kujenga mshikamano, uthubutu na kuimarisha sauti ya pamoja ya wanawake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Katika tamasha hilo lililoandaliwa na Kituo cha Redio cha Gold FM, viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi, Mbunge wa Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani na Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Benjamini Ngayiwa, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Tamasha hilo limepambwa na burudani kutoka kwa msanii mkongwe wa muziki wa taarab, Mzee Yusuph, huku uendeshaji wa shughuli ukifanywa na MC maarufu Dkt. Kumbuka na mtaalamu wa maendeleo ya familia na uchumi, Dkt. Chris Mauki, aliyetoa mada mbalimbali zilizolenga kuwainua wanawake kiuchumi na kijamii.

Aidha, jumla ya tuzo tisa za ushindani zimetolewa kwa washindi waliopatikana kupitia kura za wananchi, pamoja na tuzo maalum za heshima na vyeti kwa wadau waliotoa mchango mkubwa katika kuwawezesha wanawake.

Tuzo hizo zimetolewa kwa wanawake waliobobea katika nyanja mbalimbali zikiwemo ujasiriamali, madini, ubunifu, ushonaji, upishi, saluni pamoja na wanawake wenye ushawishi chanya katika jamii, hatua inayolenga kuhamasisha wanawake wengine kujituma na kufikia mafanikio.

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano lililofanyika Aprili 11, 2026 katika Ukumbi wa Malex uliopo Kahama, mkoani Shinyanga - Picha na Kadama Malunde -  Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano lililofanyika Aprili 11, 2026 katika Ukumbi wa Malex uliopo Kahama, mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano lililofanyika Aprili 11, 2026 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akiimba na kucheza na Wanawake Chuma  kwenye Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizindua kikundi cha Wanawake Chuma katika  Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akikabidhi katiba ya kikundi cha Wanawake Chuma katika  Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akikata keki katika  Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano
Mwandaaji wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2026 ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Redio cha Gold FM, Bi. Neema Mghen akisoma risala kuhusu Tamasha la Mwanamke Chuma
Mwandaaji wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2026 ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Redio cha Gold FM, Bi. Neema Mghen akisoma risala kuhusu Tamasha la Mwanamke Chuma
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza katika Tamasha la Mwanamke Chuma 2026
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Benjamini Ngayiwa akizungumza katika Tamasha la Mwanamke Chuma 2026
Mwandaaji wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2026 ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Redio cha Gold FM, Bi. Neema Mghen akikabidhi tuzo ya Heshima kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi
Mtaalamu wa maendeleo ya familia na uchumi, Dkt. Chris Mauki akitoa mada kwenye tamasha la Mwanamke Chuma 2026 
Mtaalamu wa maendeleo ya familia na uchumi, Dkt. Chris Mauki akitoa mada kwenye tamasha la Mwanamke Chuma 2026 
Msanii Mkongwe wa Taarabu, Mzee Yusuph akitoa Burudani
Msanii Mkongwe wa Taarabu, Mzee Yusuph akitoa Burudani

















No comments:

Post a Comment