REA MMEBEBA AJENDA YA RAIS SAMIA- SUBIRA MGALU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 23, 2026

REA MMEBEBA AJENDA YA RAIS SAMIA- SUBIRA MGALU


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inaridhishwa na namna ambavyo Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza miradi ya Kusambaza Nishati Vijijini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu amesema hayo Aprili 22, 2026 alipotembelea Banda la REA kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

"REA mmeibeba vyema ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Nishati Safi ya Kupikia inawafikia wananchi wengi wa Vijijini," amesema Mhe. Mgalu

Amesisitiza uhamasishaji na Elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia iendelee kutolewa ili kufanikisha lengo la Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Amesema Kamati anayoiongoza pamoja na Wabunge wataendelea kuwa mabalozi wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwani tayari wanao uelewa wa kutosha.

Aidha, kuhusu suala la usambazaji wa umeme, Mhe. Mgalu amesema kazi kubwa imetekelezwa na REA kwani tayari vijiji vyote nchini vimefikishiwa umeme na kwamba Miradi inaendelea kutekelezwa ya kufikisha vitongojini.

Kwa nyakati tofauti, Wabunge waliotembelea Banda la REA walieleza kuridhishwa kwao na hatua za utekelezaji wa miradi zinazoendelea kuchukuliwa na REA.

No comments:

Post a Comment