
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amepokea taarifa ya washindi wa shindano la Ubunifu kwa Wanafunzi Challenge linalohusu namna ya kupunguza tatizo la msongamano wa magari mijini. Taarifa hiyo imewasilishwa leo, tarehe 28 Aprili 2026, katika Ofisi za Wizara, mkoani Dodoma.
Ikumbukwe kuwa lengo la shindano hilo ni kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu kuoanisha masomo ya kihandisi na uhalisia wa changamoto zinazoikumba jamii, hususan katika miji mikubwa inayokumbwa na tatizo la foleni.
Takribani maandiko 561 kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi yalipokelewa na kufanyiwa kazi na Kamati maalum ya shindano hilo.



No comments:
Post a Comment