USHIRIKIANO WA SEKTA CHACHU YA MAFANIKIO YA AFYA MOJA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 29, 2026

USHIRIKIANO WA SEKTA CHACHU YA MAFANIKIO YA AFYA MOJA.



NA, Mwandishi wetu – Muleba, Kagera


Timu ya wataalam kutoka sekta za afya, mifugo, mazingira, wanyamapori na kilimo imekutana katika Halmashauri ya Wilaya ya muleba mkoani Kagera kwa lengo la kuandaa Mpango wa Mkoa wa Afya Moja ambao utatumika kubaini rasilimali zitakazosaidia kutatua changamoto na vihatarishi vya afya ya binadamu, wanyama na mazingira.

Afya Moja inawaleta wadau pamoja kwa lengo la kuunganisha nguvu kutoka sekta mbalimbali ili kuhakikisha dhana hiyo inatekelezwa kwa matendo huku ikizaa matunda yanayotarajiwa kwa kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwake.

Ofisi ya Waziri Mkuu yenye jukumu la kuratibu shughuli za Serikali, imebeba dhana hiyo kwa kuhakikisha inawashirikisha wadau wote muhimu huku ikiwa kinara katika kuivusha dhana ya Afya Moja Nchini.







No comments:

Post a Comment