Amesema hayo alipotembelea na kukagua eneo litakalojengwa uwanja wa michezo wa Ofisi ya Makamu wa Rais lililopo Ipala jijini Dodoma leo Mei 08, 2026.
Dkt. Muyungi alisema kuwa uwanja huo ukikamilika utatoa fursa kwa taasisi zingine kupata maeneo ya michezo.
Aliongeza kuwa uwanja huo utakapokamilika utakuwa ni chachu kwa watumishi wa Ofisi hiyo kuimarisha ushirikiano na taasisi zingine kupitia michezo.
"Kama tunavyofahamu michezo si tu burudani bali ni sehemu ya kulinda afya zetu kupitia mazoezi mbalimbali ya viungo," alisema.
Katika ziara hiyo Dkt. Muyungi aliambatana na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda na Menejimenti ya Ofisi hiyo.






No comments:
Post a Comment