MKENDA: ELIMU JUMUISHI KUENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 7, 2026

MKENDA: ELIMU JUMUISHI KUENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE




Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA


Serikali imeendelea kuimarisha elimu jumuishi nchini kwa kununua na kusambaza vifaa mbalimbali vya kielimu na saidizi kwa walimu, wakufunzi na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule na vyuo vya ualimu.

Hayo yameelezwa bungeni jijini na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Prof. Mkenda amesema vifaa vilivyonunuliwa na kusambazwa ni pamoja na kompyuta mpakato 688, mashine za kidijitali za kurekodi sauti 377, tablets 196, mashine za Breili za kielektroniki 19, emboza sita, mashine saba za kuongeza sauti pamoja na seti nne za kupima usikivu.

Amesema vifaa hivyo vimesambazwa katika shule za msingi 309, shule za sekondari 629 pamoja na vyuo vya ualimu 10 kwa lengo la kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, wanufaika wa vifaa hivyo ni pamoja na watu wenye ulemavu wa viungo 342, wenye changamoto ya uoni 312, wenye uziwi 155, wenye ualbino 190 pamoja na wenye usikivu hafifu 198.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kuimarisha huduma za elimu jumuishi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata fursa sawa ya elimu bila kujali changamoto walizonazo.

No comments:

Post a Comment