TRA KARIAKOO YATEMBELEA KIJIWE CHA RAHA SQUARE NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 6, 2026

TRA KARIAKOO YATEMBELEA KIJIWE CHA RAHA SQUARE NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI

Wafanyabiashara Wa Kijiwe cha Raha Square Wamepata Fursa Ya Kukutana Na Kaimu Meneja Wa Kariakoo Bw.Edson Issanya, ambapo waliwasilisha changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kikodi, ikiwemo uelewa mdogo wa masuala ya kodi.

Kupitia ziara hiyo, walipakodi walieleza maoni yao moja kwa moja na kupata ufafanuzi pamoja na mwongozo sahihi kutoka TRA juu ya namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo ili kuongeza uelewa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza Katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Bw. Severine Mushi, ameshukuru na kupongeza jitihada za TRA za kuwafikia moja kwa moja, akieleza kuwa hatua hiyo imewasaidia kupata uelewa wa masuala ya kodi kwa wakati na kuimarisha uhusiano kati ya TRA na wafanyabiashara.

Na alisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo, akipendekeza kuwepo kwa vikao maalum na mabalozi wa nyumba ili kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kuongeza uelewa na kuboresha utekelezaji wa masuala ya kodi.

Aidha, TRA imeendelea kuonesha dhamira ya kuboresha huduma kwa walipakodi kwa kuweka mikakati mbalimbali, ikiwemo utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango, kuhamasisha usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), pamoja na kuimarisha ushirikiano na wafanyabiashara.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuwasogezea huduma walipakodi na kujenga uelewa wa kodi.

No comments:

Post a Comment