Na Okuly Julius ,OKULY BLOG,DODOMA
Wanafunzi 22,500 wanatarajiwa kunufaika na elimu ya stadi za maisha, ujuzi na elimu ya msingi kupitia Programu ya Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Mfumo Rasmi ifikapo mwaka 2027, ikiwa ni ongezeko kutoka vijana 16,732 mwaka 2026.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/27.
Serikali imesema itaendelea kuimarisha elimu nje ya mfumo rasmi ili kutoa fursa kwa vijana waliokosa nafasi katika mfumo rasmi kutokana na sababu mbalimbali, ambapo idadi ya wanafunzi wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala itaongezeka kutoka 14,765 mwaka 2025/26 hadi 16,000 mwaka 2026/27.
Katika hatua nyingine, Serikali itaendelea kuimarisha elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kuboresha huduma za ubainishaji, upimaji na utoaji wa elimu nyumbani.
Aidha, wakufunzi 100 kutoka VETA za mikoa na vyuo vya maendeleo ya wananchi watapatiwa mafunzo maalum kuhusu kuwahudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum, sambamba na mafunzo kwa maafisa elimu maalum 52, maafisa uthibiti ubora wa shule 52 na wakuu wa shule 52 kuhusu ubainishaji na upimaji wa wanafunzi hao.
Kwa upande wa maendeleo ya fasihi, Serikali itaendelea kuratibu na kusimamia Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu kwa lengo la kuhamasisha uandishi wa kazi za fasihi ya Kiswahili ikiwemo riwaya, hadithi fupi na ushairi, hatua inayolenga kukuza tasnia ya uandishi nchini na kuwajengea uwezo waandishi chipukizi.

No comments:
Post a Comment