
Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Sophia Kibaba akimkabidhi fomu Dk. Fabian Madele ya kuomba idhini ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) .

Dk. Fabian Madele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba idhini ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Dk. Fabian Madele akionesha fomu ya kuomba idhini ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
Na Okuly Julius – Dodoma
LEO, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kujitokeza kuchukua fomu za kuomba idhini ya kuwania nafasi za ubunge na udiwani katika majimbo ya Dodoma Mjini na Mtumba, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Miongoni mwa waliojitokeza ni Dk. Fabian Madele, mshauri wa Rais, ambaye amesema ameamua kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo la Dodoma Mjini kupitia CCM, akitumia haki yake ya kikatiba na dhamira ya dhati ya kulitumikia jimbo hilo.
“Leo nimetumia haki yangu ya kikatiba kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi kwa Jimbo la Dodoma Mjini,” amesema Dk. Madele mara baada ya kuchukua fomu hiyo.
Ameongeza kuwa: “Nimekuwa na dhamira ya dhati kutoka moyoni mwangu kuchukua fomu hii, ili panapo majaliwa nikipata nafasi niwatumikie wananchi wa Dodoma Mjini kwa nafasi ya ubunge.”
Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu unatarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa, huku ukihusisha wanachama mbalimbali wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kupitia CCM katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma.
No comments:
Post a Comment