TISEZA YATEMBELEA KONGANI YA BUZWAGI NA KUPONGEZA BARRICK KWA MCHAKATO WA KUFUNGA MGODI WA VIWANGO VYA KIMATAIFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 18, 2025

TISEZA YATEMBELEA KONGANI YA BUZWAGI NA KUPONGEZA BARRICK KWA MCHAKATO WA KUFUNGA MGODI WA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ulipata fursa kutembelea maeneo ya wawekezaji mbalimbali kwenye eneo la Kongani ya Buzwagi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bw.Gilead John Teri akiongea na  kamati ya Utekelezaji wa Kongani ya Buzwagi na wafanyakazi wa Barrick baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya kutembelea eneo hilo.
Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi (aliyenyosha mkono)  akitembeza ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Kongani ya Buzwagi.
Ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ulipata fursa kutembelea maeneo ya wawekezaji mbalimbali kwenye eneo la Kongani ya Buzwagi.
Meneja Utekelezaji wa Mradi  wa Kongani ya Buzwagi  kutoka Barrick, Stanley Joseph akifanya wasilisho kwa ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) uliofanya ziara mgodini hapo.

**
Ujumbe wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ukiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu Bw. Gilead John Teri umefanya ziara ya kikazi katika eneo la mgodi wa Barrick Buzwagi uliofungwa baada ya kumalizika muda wa uchimbaji ambalo limebadilishwa kuwa Kongani ya Buzwagi na kuridhishwa na mchakato mzima unaoendelea wa kufunga mgodi huo.

Akiwa katika eneo hilo Gilead Teri amepata taarifa fupi ya uwekezaji wa aina mbalimbali ndani ya Buzwagi Special Economic Zone na kukagua maeneo mbalimbali yatakayotumiwa na wawekezaji watakaohitaji kuwekeza katika Kongani hiyo na ametembelea kiwanda cha kuzalisha Conveyor ambacho tayari kimeanza kufanya uzalishaji sambamba na kuzalisha fursa za ajira.

Akiongea baada ya ziara hiyo, Bw. Teri ametoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali kwa kufanikisha ufungaji wa mgodi huo kwa viwango vya kimataifa ambapo sasa umegeuka kuwa sehemu ya kimkakati wa kukuza uchumi wa nchi kupitia uwekezaji katika sekta ya viwanda na biashara.

“Nawapongeza Barrick kwa kuhakikisha mgodi huu unafungwa kitaalamu pia naipongeza kamati ya Utekelezaji wa Kongani hii inavyofanya kazi na kushirikiana na mamlaka mbalimbali lengo likiwa kutimiza kufanikisha lengo la Serikali la kuhakikisha eneo hili linatumika kimkakati ili liweze kuendelea kuleta manufaa kwa taifa”,amesema Teri.

Teri pia amesema ameridhishwa na kampeni za kutangaza eneo hilo zinazoendelea ambazo zinabainisha fursa zilizopo na mipango iliyowekwa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma kwa kuhakikisha huduma zote kutoka taasisi mbalimbali zinapatikana katika eneo moja yaani One Stop Centre.

Kwa upande wake, Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi, amesema tayari eneo hilo la kongani ya Buzwagi limepatiwa usajiri na serikali kwa ajili ya shughuli hiyo ya Kongani na likikamilika hali litawezesha kupatikana ajira nyingi kwa vijana wa mkoa wa shinyanga na Tanzania kiujumla sambamba na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Aidha Mumbi ameeleza ujumbe huo kuwa hadi kufikia sasa wawekezaji 19 wameonyesha nia ya Kuwekeza katika Kongani hiyo huku wawekezaji 5 tayari wameanza mchakato wa usajili na tayari mwekezaji mmoja ameishaanza uzalishaji .

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, alitoa wito kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kuweka msisitizo katika kutangaza mradi mkubwa wa Kongani ya Uwekezaji Buzwagi, ambao unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Aidha, RC Mboni alibainisha kuwa Shinyanga ipo tayari kupokea wawekezaji kwa sasa kutokana na mazingira wezeshi yaliyowekwa na Serikali kutokana na mkoa kuwa na raslimali zote muhimu kwa uwekezaji ikiwemo ardhi kubwa na salama kwa uwekezaji, upatikanaji wa maji na nishati ya umeme wa uhakika, miundombinu ya kisasa ikiwa ni pamoja na barabara, uwanja wa ndege wa Shinyanga na Kahama, na mtandao wa mawasiliano ya uhakika, nguvu kazi ya kutosha na yenye ari.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bw.Gilead John Teri akiongea na  kamati ya Utekelezaji wa Kongani ya Buzwagi na wafanyakazi wa Barrick baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya kutembelea eneo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bw.Gilead John Teri akiongea na  kamati ya Utekelezaji wa Kongani ya Buzwagi na wafanyakazi wa Barrick baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya kutembelea eneo hilo.
Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi akieleza ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) jinsi mchakato  wa kubadilisha mgodi huo uliofungwa  kuwa  Kongani ya Buzwagi unavyoendelea  wakati ulipofanya ziara kwenye eneo hilo la mgodi.

Meneja wa ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi (aliyenyoosha mkono)  akitembeza ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Kongani ya Buzwagi.
Meneja Utekelezaji wa Mradi  wa Kongani ya Buzwagi  kutoka Barrick, Stanley Joseph akifanya wasilisho kwa ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) uliofanya ziara mgodini hapo.
Meneja Utekelezaji wa Mradi  wa Kongani ya Buzwagi  kutoka Barrick, Stanley Joseph akifanya wasilisho kwa ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) uliofanya ziara mgodini hapo.
Meneja Utekelezaji wa Mradi  wa Kongani ya Buzwagi  kutoka Barrick, Stanley Joseph akifanya wasilisho kwa ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) uliofanya ziara mgodini hapo.
Ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ulipata fursa kutembelea maeneo ya wawekezaji mbalimbali kwenye eneo la Kongani ya Buzwagi.
Ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ulipata fursa kutembelea maeneo ya wawekezaji mbalimbali kwenye eneo la Kongani ya Buzwagi.
Ujumbe kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ulipata fursa kutembelea maeneo ya wawekezaji mbalimbali kwenye eneo la Kongani ya Buzwagi.

No comments:

Post a Comment