TAASISI YA ATIDI YASISITIZWA KUSAIDIA SEKTA BINAFSI KUELEKEA DIRA 2050 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 25, 2026

TAASISI YA ATIDI YASISITIZWA KUSAIDIA SEKTA BINAFSI KUELEKEA DIRA 2050

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akitoa rai kwa ujumbe wa Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo, Prof. Kelly Kingsly, kushirikiana na Tanzania hususani kwa Sekta binafsi ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akikabidhiwa Cheti na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI) Prof. Kelly Kingsly, baada ya mkutano kati yao uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI) Prof. Kelly Kingsly, baada ya mkutano kati yao uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI), Prof. Kelly Kingsly, akieleza lengo la Taasisi hiyo la kusaidia kuweka mazingira bora zaidi ya ufanyaji biashara, wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), uliofanyika Ofisi za Wizara ya Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.
Ujumbe wa Wizara ya Fedha ukiwa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) Mwenyekiti wa Bodi ya Bodi ya Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI), Prof. Kelly Kingsly, kuhusu ushirikiano na Taasisi hiyo, katika Ofisi za Wizara ya Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.
Ujumbe wa Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI), ukiwa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) Mwenyekiti wa Bodi ya Bodi ya Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI), Prof. Kelly Kingsly, kuhusu ushirikiano na Taasisi hiyo, katika Ofisi za Wizara ya Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI) Bw. Manuel Moses, baada ya mkutano kati yao uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiongoza mkutano kati yake na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI) Prof. Kelly Kingsly, kuhusu ushirikiano na Taasisi hiyo katika Ofisi za Wizara ya Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.

Na. Jordan Mbwambo na Peter Haule, WF, Dodoma


Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) ametoa rai kwa Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI) kushirikiana na Tanzania hususani katika kukuza Sekta binafsi ili nchi iweze kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050.

Rai hiyo ameitoa wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Taasisi ya ATIDI ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo, Prof. Kelly Kingsly, yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma

Mhe. Balozi Omar, alisema kuwa katika Dira ya Taifa, 2050 sekta binafsi imekusudiwa kuichangia asilimia 70 ya uchumi na asilimia 30 itachangiwa na sekta ya umma jambo linalohitaji kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili itoe mchango huo kwa ufanisi.

“Utekelezaji wa Dira 2050 unaenda sambammba na kuendeleza sekta binafsi kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji, katika hilo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliunda Tume iliyotoa mapendekezo ya Maboresho ya Mfumo wa Kodi nchini ambayo tayari imewasilisha mapendekezo hayo kwa Mhe. Rais”, alisema Mhe. Balozi Omar.

Alisema kuwa Taasisi ya ATIDI ni muhimu Barani Afrika hususani katika masuala ya kukabiliana na vihatarishi barani Afrika ikiwemo Tanzania kwa kuwa kuna idadi ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwa kushirikiana na Taasisi hiyo, zikiwemo sekta za biashara na uwekezaji.

Aidha, alisema kuwa Sekta ya fedha pia ina mchango mkubwa katika kufikia malengo hayo kwa kutengeneza mazingira ya uchumi jumuishi utakao kuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Bima ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji Afrika (ATIDI), Prof. Kelly Kingsly, alisema kuwa Taasisi yake itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania kwa kuunga mkono biashara za ndani, kuweka mkazo kwenye kujenga uwezo wa wafanyakazi ili kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na sifa stahiki.

Prof. Kingsly alisema kuwa Taasisi inazingatia masuala ya uwekezaji, maarifa ya kimkakati na inachukua jukumu la utetezi wa sera kwa kuona namna bora ya kuunda mazingira rafiki zaidi ya biashara.

Alisema hatua hizo zinalenga kujenga mazingira wezeshi ya biashara kwa kuzingatia Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals – SDGs), ambayo ndiyo Dira Kuu ya kufikia malengo yaliyowekwa.

“Sote tuliridhia Malengo ya Maendeleo Endelevu na tunatarajia kwamba kwa upande wa utekelezaji, tutaendelea kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya miundombinu na maendeleo kwa ujumla kwa kuzingatia mwelekeo huo”, alisema Prof. Kingsly

Vilevile alisema kuwa, ili Serikali ipate thamani halisi ya uwekezaji wake wa kifedha, ni muhimu kutumia ipasavyo Mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP – Public-Private Partnerships) kwa kuwa Mfumo huo hautasaidia tu kuongeza rasilimali, bali pia utachochea ubunifu unaohitajika pamoja na maendeleo yanayotarajiwa.

No comments:

Post a Comment