MBUNGE NASRIYA AOMBA LUGHA YA ALAMA KUWA SOMO RASMI NGAZI ZOTE ZA ELIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 8, 2026

MBUNGE NASRIYA AOMBA LUGHA YA ALAMA KUWA SOMO RASMI NGAZI ZOTE ZA ELIMU


Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA 


Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Nasriya Nasir Ali ameiomba Serikali kuhakikisha lugha ya alama inafundishwa kama somo rasmi katika ngazi zote za elimu nchini ili kuimarisha ujumuishaji katika sekta ya elimu.

Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bungeni jijini Dodoma, Nasriya ameipongeza Wizara hiyo kwa kuandaa bajeti inayolenga kutoa fursa sawa na kujumuisha watu wenye ulemavu katika mfumo wa elimu.

Amesema hatua ya kufundisha lugha ya alama kwa upana itasaidia kuongeza mawasiliano na ushiriki wa watu wenye ulemavu wa kusikia katika jamii pamoja na kuboresha upatikanaji wa elimu jumuishi nchini.

No comments:

Post a Comment