
Bodi ya Maji ya Bonde la Wami-Ruvu kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) pamoja na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Tanzania, wameshiriki zoezi jumuishi la kuotesha miti rafiki wa maji kando ya Bwawa la Mindu, Kata ya Mindu, Manispaa ya Morogoro.
Zoezi hilo ni sehemu ya Uzinduzi wa Mradi wa Uhifadhi wa Vyanzo vya Maji katika Kidakio cha Ngerengere.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Wizara ya Maji, Bi. Rosemary Rwebugisa, ameongoza tukio hilo kwa kuotesha zaidi ya miti elfu moja, miti hiyo ina manufaa kwa jamii, ikiwemo kusaidia uhifadhi wa mazingira, kuimarisha bionuai na kulinda vyanzo vya maji.
Bi. Rwebugisa amesema hatua hiyo inalenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira, hususan vyanzo vya maji, ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali hiyo muhimu kwa maendeleo ya jamii na uchumi.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Maji wameshiriki katika zoezi hilo, wakiwamo wananchi wakazi wa eneo la Mindu, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.





No comments:
Post a Comment